Viwango Vya Mishahara Ya Watumishi wa Serikali 2025

Viwango Vya Mishahara Ya Watumishi wa Serikali 2025

#1

     Viwango vya mishahara serikalini

Viwango Vya Mishahara Ya Watumishi wa Serikali 2025 (TGS salary Scale)

Viwango Vya Mishahara Ya Watumishi wa Serikali 2025 (TGS salary Scale) 

|Mishahara ya Wafanyakazi Serikalini

Serikali inaendelea kutekeleza Sera ya 

malipo ya Mshahara na Motisha katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 2010. Katika hatua za kutimiza malengo ya Sera hii, 

Serikali imefanya marekebisho ya 

mishahara ya watumishi wake kuanzia

tarehe 1 Julai, 2022.


Kufuatia marekebisho hayo, kima cha chini cha mshahara kimeongezwa kwa asilimia 23.3 kutoka shlingi 300,000 kwa mwezi 

hadi shilingi 370,000 kwa mwezi. Ngazi nyingine za mshahara zimeongezwa kwa asilimia tofauti.

Kutokana na mabadiliko haya, upeo wa 

ngazi za mishahara iliyotolewa kwa Waraka wa Watumishi wa Serikali Na. 1 wa mwaka 2015, sasa utakuwa kama ilivyooneshwa katika Viambatanisho Na. 1 — 11 vya 

Waraka huu.


Aidha, vianzia mshahara kwa msingi wa 

Elimu, Muda wa Mafunzo, aina ya kazi na 

ujuzi vitakuwa kama vilivyoainishwa katika Miundo ya Maendeleo ya Utumishi ya kada husika pamoja na miongozo mbalimbali iliyotolewa na Ofisi hii. Marekebisho haya yanawahusu watumishi wa Serikali Kuu, watumishi wa Serikali za Mitaa, watumishi walioshikizwa kwenye Taasisi za Umma pamoja na watumishi ambao watakuwa kwenye likizo inayoambatanana na kuacha kazi au kustaafu kazi baada ya tarehe 1 

Julai, 2022.





Viwango Vya Mishahara Ya Watumishi wa Serikali 2025 (TGS salary Scale)

TGS Salary Scale ni muundo wa mishahara unaotumika kuamua malipo ya watumishi 

wa serikali katika kada mbalimbali nchini Tanzania. Muundo huu unalenga 

kuhakikisha usawa katika malipo ya watumishi, kwa kuzingatia vigezo kama 

ngazi ya elimu, uzoefu, na aina ya kazi.

Muundo huu wa mishahara ya wafanyakazi serikalini hutumika katika ngazi mbalimbali ikiwemo katika watumisho wa ngazi za 

wilaya kama vile watendaji wa mtaa, 

watendaji wa kijiji, fundi sanifu n.k. Kwa 

miaka mingi, serikali imekuwa ikifanya marekebisho ya mara kwa mara kwenye muundo huu ili kuendana na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.


Makundi ya Viwango vya Mishahara ya TGS Salary Scale

Viwango vipya vya mishahara ya Watumishi wa Serikali 2025 (TGS salary Scale) vimegawanywa katika ngazi mbalimbali 

(TGS A – TGS J), kuanzia ngazi ya chini 

kabisa (TGS A) hadi ngazi ya juu kabisa 

(TGS J).

Kila ngazi ina madaraja kadhaa ambayo yamepangwa kutokana na uzoefu wa kazi, 

na kila daraja lina kiwango chake cha mshahara. Kwa mfano, ngazi ya TGS A ina madaraja 8, kuanzia TGS A.1 hadi TGS A.8. Mshahara wa kuanzia kwa ngazi ya TGS A.1 ni Tshs. 380,000 kwa mwezi, huku mshahara 

wa juu kabisa kwa ngazi ya TGS J.1 ni Tshs. 3,380,000 kwa mwezi.


Viwango vya Mishahara ya TGS A Salary Scale

Ngazi ya MshaharaKuanzia Julai, 2022/23
TGS A.1380,000
TGS A.2388,500
TGS A.3397,000
TGS A.4405,500
TGS A.5414,000
TGS A.6422,500
TGS A.7431,000
TGS A.8439,500

Viwango vya Mishahara ya TGS B Salary Scale

Ngazi ya MshaharaKuanzia Julai, 2022/23
TGS B.1450,000
TGS B.2461,000
TGS B.3472,000
TGS B.4483,000
TGS B.5494,000
TGS B.6505,000
TGS B.7516,000
TGS B.8527,000
TGS B.9538,000
TGS B.10549,000

Viwango vya Mishahara ya TGS C Salary Scale

Ngazi ya MshaharaKuanzia Julai, 2022/23
TGS C.1585,000
TGS C.2598,000
TGS C.3611,000
TGS C.4624,000
TGS C.5637,000
TGS C.6650,000
TGS C.7663,000
TGS C.8676,000
TGS C.9689,000
TGS C.10702,000
TGS C.11715,000
TGS C.12728,000

Viwango vya Mishahara ya TGS D Salary Scale

Ngazi ya MshaharaKuanzia Julai, 2022/23
TGS D.1765,000
TGS D.2780,000
TGS D.3795,000
TGS D.4810,000
TGS D.5825,000
TGS D.6840,000
TGS D.7855,000
TGS D.8870,000
TGS D.9885,000
TGS D.10900,000
TGS D.11915,000
TGS D.12930,000

Viwango vya Mishahara ya TGS E Salary Scale

Ngazi ya MshaharaKuanzia Julai, 2022/23
TGS E.11,000,000
TGS E.21,019,000
TGS E.31,038,000
TGS E.41,057,000
TGS E.51,076,000
TGS E.61,095,000
TGS E.71,114,000
TGS E.81,133,000
TGS E.91,152,000
TGS E.101,171,000
TGS E.111,190,000
TGS E.121,209,000

Viwango vya Mishahara ya TGS F Salary Scale

Ngazi ya MshaharaKuanzia Julai, 2022/23
TGS F.11,300,000
TGS F.21,324,000
TGS F.31,348,000
TGS F.41,372,000
TGS F.51,396,000
TGS F.61,420,000
TGS F.71,444,000
TGS F.81,468,000
TGS F.91,492,000
TGS F.101,516,000
TGS F.111,540,000
TGS F.121,564,000

Viwango vya Mishahara ya TGS G Salary Scale

Ngazi ya MshaharaKuanzia Julai, 2022/23
TGS G.11,660,000
TGS G.21,691,000
TGS G.31,722,000
TGS G.41,753,000
TGS G.51,784,000
TGS G.61,815,000
TGS G.71,846,000
TGS G.81,877,000
TGS G.91,908,000
TGS G.101,939,000
TGS G.111,970,000
TGS G.122,001,000

Viwango vya Mishahara ya TGS H, I & J Salary Scale

Ngazi ya MshaharaKuanzia Julai, 2022/23
TGS H.12,110,000
TGS H.22,172,000
TGS H.32,234,000
TGS H.42,296,000
TGS H.52,358,000
TGS H.62,420,000
TGS H.72,482,000
TGS H.82,544,000
TGS H.92,606,000
TGS H.102,668,000
TGS H.112,730,000
TGS H.122,792,000
TGS I.12,905,000
TGS I.23,022,000
TGS I.33,139,000
TGS I.43,256,000
TGS J.13,380,000

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code