MAAJABU:Kudungwa manii ya samaki usoni kama aina ya Urembo je ni Salama?
Mtaalamu mshauri wa magonjwa ya ngozi Dk John Pagliaro, aliyeko Brisbane, Australia, anasema kwamba ingawa tunajua kuwa nyukleotidi zina jukumu muhimu katika miili yetu - ndizo nyenzo za ujenzi wa DNA yetu kwa mwanzo - anahoji ikiwa "kudunga sindano zenye DNA ya salmoni iliyokatwa vipande vidogo vidogo" kwenye nyuso zetu kutafanya kazi pamoja na nyukleotidi zetu wenyewe.
"Hatuna data nzuri, yenye nguvu," anasema. "Kama mtaalamu wa matibabu, ningetaka kufuatilia angalau miaka michache zaidi ya tafiti kubwa, za kuaminika zinazoonyesha usalama na ufanisi kabla sijaanza kuitumia katika kazi yangu. Ukweli ni kwamba bado hatujafikia hitimisho." Via BBC









image quote pre code