Lyle Gittens na Eleanor Gittens wavunja Rekodi kuwa wanandoa wenye ndoa ndefu zaidi duniani

Lyle Gittens na Eleanor Gittens wavunja Rekodi kuwa wanandoa wenye ndoa ndefu zaidi duniani

#1

Lyle Gittens (108) na Eleanor Gittens (107) wametambuliwa rasmi kuwa wanandoa wenye ndoa ndefu zaidi duniani baada ya kutimiza miaka 83 ya ndoa. Rekodi yao imethibitishwa kupitia kumbukumbu mbalimbali za kihistoria, zikionyesha safari yao ya maisha iliyojaa upendo, uvumilivu na ushikamano wa kipekee.

Wawili hao walikutana mwaka 1941 kwenye mchezo wa mpira wa kikapu wakiwa chuoni, na mwaka mmoja baadaye 1942 walifunga ndoa wakati Lyle akiwa kwenye mapumziko mafupi ya jeshi kabla ya kutumwa vitani nchini Italia. Wakati huo, Eleanor, akiwa mjamzito, aliendelea kufanya kazi New York huku wawili hao wakiwasiliana kupitia barua zilizopitiwa na jeshi kutokana na usiri wa kivita.

Baada ya vita kumalizika, Lyle alirejea Marekani na wanandoa hao wakaanza kujenga maisha yao upya jijini New York. Walihitimu masomo ya juu, kusafiri sehemu mbalimbali duniani na hatimaye kuhamia Miami walikostawi na kuishi maisha ya utulivu.

Wanapoulizwa siri ya mafanikio ya ndoa yao ya zaidi ya nusu karne, Lyle na Eleanor hutaja kauli moja rahisi lakini yenye nguvu: "Tunapendana."

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code