Mashambulizi ya Ukraine dhidi ya Urusi usiku wa kuamkia Jumapili, yamesababisha kukatika kwa umeme katika miji mikubwa miwili mpakani mwa nchi hizo. Mamlaka za Urusi zimesema takriban watu 20,000 hawana umeme kutokana na mashambulizi hayo
Gavana wa mkoa Belgorod Gavana Vyacheslav Gladkov amesema mfumo wa usambazaji wa umeme umepata madhara makubwa. Naye Gavana wa Voronezh, Alexander Gusev ameeleza kuwa, shambulio la droni kwenye mkoa wake lilisababisha kukatika kwa umeme kwa muda kwenye baadhi ya maeneo.
Katika mkoa wa magharibi wa Kursk, moto mkubwa uliibuka katika moja ya mitambo ya kufua umeme kwenye kijiji cha Korenevo na kusababisha maeneo 10 kukosa umeme.
Miundombinu ya umeme yaharibiwa Ukraine
Wakati huo huo Ukraine imeripoti mashambululizi kadhaa ya droni na makombora yaliyofanywa na Urusi yaliyoilenga miundombinu yake ya umeme. Mamlaka nchini humo zimesema zimefanikiwa kuzizuia droni 34 kati ya 69 usiku wa kuamkia Jumapili.
Hayo yanaendelea wakati Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetangaza kuwa vikosi vyake sasa vinalidhibiti eneo la Rybne katika mkoa wa Zaporizhzhia









image quote pre code