Muigizaji wa Hollywood Spencer Lofranco, nyota wa filamu za Jamesy Boy na Gotti, afariki akiwa na umri wa miaka 33
Muigizaji wa Hollywood Spencer Lofranco, anayejulikana Zaidi kwa uigizaji wake katika filamu za Jamesy Boy, Gotti, na Unbroken, amefariki akiwa na umri wa miaka 33.
Mamlaka huko British Columbia, Kanada, kwa sasa wanachunguza kifo chake, na chanzo hakijathibitishwa.
Ndugu yake Lofranco, Santino Lofranco, alitangaza habari hiyo ya kuhuzunisha kwenye Instagram, akiandika:
“Ndugu yangu… Uliishi maisha ambayo wengine wangeweza kuyaota. Ulibadilisha maisha ya watu, na sasa uko na Mungu. Nitakupenda na kukukumbuka daima Bear. Lala salama. Oktoba 18, 1992 – Novemba 18, 2025.”







image quote pre code