Mwandishi habari wa Uingereza kuachiliwa kutoka kizuizini Marekani

Mwandishi habari wa Uingereza kuachiliwa kutoka kizuizini Marekani

#1

Mwanahabari wa Uingereza Sami Hamdi anatazamiwa kuachiliwa kutoka kizuizini nchini Marekani wiki mbili baada ya kuzuiliwa na Idara ya uhamiaji, familia yake ilisema Jumatatu.

Idara ya Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha ya Marekani (ICE) ilimkamata Hamdi, mchambuzi wa vyombo vya habari na mkosoaji mkubwa wa Israel, mwezi uliopita alipokuwa katika ziara nchini Marekani.

Wizara ya Mambo ya Nje na Idara ya Usalama wa Ndani (DHS) ilidai wakati huo Hamdi anaunga mkono ugaidi na ni tishio kwa usalama wa taifa, huku mawakili wake wakidai kwamba alilengwa kwa kukosoa Israeli na vita vilivyokuwa vikiendelea huko Gaza.

Hamdi ataachiliwa kutoka kizuizini siku chache zijazo na kurejea Uingereza, wawakilishi wake wanasema.

Hamdi alikuwa akizuru Marekani kwa ajili ya kuhutubia hafla za Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR), kikundi cha kutetea Waislamu, wakati maafisa wa ICE walipomkamata kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa San Francisco tarehe 26 Oktoba.

Kuzuiliwa kwake kulikuja baada ya serikali ya Marekani kubatilisha visa ya Hamdi na ukosoaji kutoka kwa mwanaharakati wa siasa kali za mrengo wa kulia na mshirika wa Trump Laura Loomer, ambaye alimshutumu kwa kuunga mkono magaidi

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code