Ndani ya juhudi za Kenya za kutokomeza kichocho ifikapo 2030
Paul Ochieng anaanza siku zake mapema saa 12 asubuhi. Yeye ni mkulima wa mpunga huko Ahero. Lakini wanakijiji wake wanamwita ‘daktari’ wa jamii, jina ambalo wanawapa wataalamu wa afya ya jamii (CHP).
Akiwa CHP, hubeba mkoba mdogo, kitabu cha kumbukumbu, fimbo ya kupimia ya mbao, na kuvaa koti la kuakisi la bluu au kijani.
Leo, anawakumbusha wazazi kuwaruhusu watoto wao kuhudhuria zoezi la utoaji wa dawa kwa wingi (MDA) katika Kituo cha Afya cha Hongo Ogosa kilicho karibu huko Ahero, Kaunti ya Kisumu.
“Ninapofika kwenye makazi, mimi huelezea kila familia kilichonipeleka huko. Tuna ombi la kuwaruhusu watoto kuja kuchukua dawa (Praziquantel) kutibu na kuzuia ugonjwa wa Kichocho (Bilharzia), ambao husababisha watu kukojoa damu. Dawa hii hutolewa kwa watoto wa miaka mitano hadi 15,” anasema.
Kufikia katikati ya asubuhi, zaidi ya watoto 100 husimama kwenye foleni anapoangalia urefu wao na kutoa tembe chungu, moja baada ya nyingine. "Wanatuamini kwa sababu sisi pia tunatibu malaria, kwa hivyo wametuzoea."
Kile ambacho Ochieng na CHP wengine kadhaa wanafanya ni sehemu ya juhudi za kitaifa za kuondoa moja ya magonjwa sugu zaidi nchini Kenya: kichocho, kinachojulikana pia kama (Bilharzia).










image quote pre code