Nyota wa Argentina na gwiji wa FC Barcelona, Lionel Messi, ametembelea uwanja wa Barcelona  Spotify Camp Nou

Nyota wa Argentina na gwiji wa FC Barcelona, Lionel Messi, ametembelea uwanja wa Barcelona Spotify Camp Nou

#1

Nyota wa Argentina na gwiji wa FC Barcelona, Lionel Messi, ametembelea uwanja wa Barcelona  Spotify Camp Nou usiku wa jana, ikiwa ni mara yake ya kwanza kukanyaga uwanja huo tangu aondoke mwaka 2021.

Messi, ambaye kwa sasa anachezea Inter Miami ya Marekani, ameeleza hisia zake kupitia ukurasa wake wa Instagram, akionyesha namna anavyoukumbuka uwanja huo ambao ulimpa mafanikio makubwa katika maisha yake ya soka.

 “Usiku wa jana nimerudi mahali ambapo nalipa-Miss kwa roho yangu yote. Mahali ambapo nilikuwa mwenye furaha isiyoelezeka, mliponifanya nijisikie kuwa mtu mwenye furaha zaidi duniani mara elfu. Natumai siku moja nitarudi tena  na siyo tu kuaga kama mchezaji, kwani sikuweza kufanya hivyo,” ameandika Messi.

Ujumbe huo wa Messi umeenea kwa kasi mitandaoni, ukiwapa faraja mashabiki wa Barcelona duniani kote ambao wamekuwa wakiota kumwona akirudi Camp Nou.

Katika kipindi chake cha takriban miaka 20 akiwa na Barcelona, Messi alijipatia heshima kubwa kama mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo, akishinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji kumi ya La Liga.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code