Seneta wa Marekani John Fetterman amelazwa hospitalini baada ya kuanguka

Seneta wa Marekani John Fetterman amelazwa hospitalini baada ya kuanguka

#1

Seneta wa Marekani John Fetterman amelazwa hospitalini baada ya kuanguka, ikiwa ni dharura yake ya 4 ya kimatibabu tangu aingie madarakani.

Seneta wa chama cha Democratic cha Pennsylvania John Fetterman anapokea huduma katika hospitali ya Pittsburgh baada ya kuanguka karibu na nyumba yake, kulingana na ofisi yake.

Fetterman, ambaye alianguka wakati wa matembezi ya asubuhi karibu na nyumba yake Braddock, alipelekwa hospitalini "kwa tahadhari kubwa," na anaendelea vizuri na anafanyiwa uchunguzi wa kawaida, msemaji huyo alisema.

"Baada ya tathmini, ilibainika kuwa alikuwa na mtetemeko wa ventrikali(ventricular fibrillation flare-up) uliosababisha Seneta Fetterman kuhisi kizunguzungu, akianguka chini na kujipiga usoni na majeraha madogo," msemaji wake alisema katika taarifa Alhamisi.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code