TANZIA:Aliyekuwa makamu wa rais wa Marekani Dick Cheney aaga dunia
Makamu wa rais wa zamani wa Marekani Dick Cheney amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84. Cheney alikuwa makamu wa rais wa 46, akihudumu chini ya rais Mrepublican George W. Bush kwa mihula miwili kati ya 2001 na 2009.
Cheney alikuwa makamu wa rais wa 46, akihudumu chini ya rais Mrepublican George W. Bush kwa mihula miwili kati ya 2001 na 2009. Vyombo vya habari vya Marekani vikiinukuu familia yake vimesema mbunge huyo wa zamani na waziri wa ulinzi "alifariki kutokana na matatizo ya homa ya mapafu na ugonjwa wa moyo na mishipa".
Cheney anachukuliwa kuwa mmoja wa makamu wa rais wenye nguvu zaidi katika historia ya Marekani, ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa nyuma ya pazia. Anazingatiwa na wengi kuwa mmoja wa watu waliokuwa nyuma ya uamuzi wa Marekani kuivamia Iraq kufuatia mashamabulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 yaliyofanywa na Al-Qaeda katika miji ya New York na Washington. Madai yake yasiyo sahihi kwamba Saddam Hussein alikuwa na silaha za maangamizi yalichochea kauli za vita kabla ya uvamizi wa Marekani wa 2003 dhidi ya Iraq.
Taarifa ya familia imesema "Kwa miongo kadhaa, Dick Cheney alilihudumia taifa la Marekani, ikiwa ni pamoja na wadhifa wa Mkuu wa Utumishi katika Ikulu ya White House, mwakilishi wa jimbo la Wyoming, Waziri wa Ulinzi, na Makamu wa Rais wa Marekani."





.jpeg)


image quote pre code