TANZIA:MC Pilipili amefariki dunia Leo November 16
Msanii wa Vichekesho ambaye pia ni MC, Emmanuel Mathias maarufu kama MC Pilipili amefariki dunia leo November 16 2025, baadhi ya Marafiki zake wa karibu wameithibitishia AyoTV ambapo mwili wake upo kwenye Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa sasa, AyoTV inaendelea kufuatilia kufahamu zaidi chanzo cha kifo chake.
Taarifa zinaeleza kuwa, MC Pilipili alisafiri kuelekea jijini Dodoma ambapo jioni ya leo alitarajiwa kwenda kufanya kazi yake ya ushereheshaji jijini humo, lakini akafikwa na mauti.
Global TV imezungumza na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya General, Dodoma, Ernest Ibenzi ambaye amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa MC Pilipili amefikishwa hospitalini hapo akiwa tayari amefariki dunia.









image quote pre code