Rais Donald Trump wa Marekani ametia saini mswada wa ufadhili wa kufungua tena shughuli za serikali ya Marekani na kumaliza mkwamo ambao umeshuhudiwa kwa muda mrefu zaidi katika historia ya nchi hiyo.
"Nchi haijawahi kuwa katika hali nzuri zaidi," rais anasema kabla tu ya kutia saini mswada huo.
"Ni siku njema," Trump aliendelea kusema wakati waandishi wa habari wanatolewa nje ya Ikulu.
Mswada huo utarejesha wafanyikazi wa serikali kazini, kutoa pesa kwa mashirika ya serikali, programu na idara na kurejesha malipo kwa mamia ya maelfu ya wafanyikazi ambao hawajalipwa tangu kuanza kwa mkwamo huo tarehe 1 Oktoba.
Kusimamishwa kwa shughuli za serikali kumeendelea kwa siku 43, ikipita rekodi ya hapo awali ya siku 35 - ambayo ilitokea wakati wa muhula wa kwanza wa Trump.









image quote pre code