Tukio:Kufuatia Mvua kubwa,Watu 90 wafariki kwa mafuriko Indonesia

Tukio:Kufuatia Mvua kubwa,Watu 90 wafariki kwa mafuriko Indonesia

#1

Mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yamesababisha vifo vya takriban watu 90 nchini Indonesia wiki hii huku mvua kubwa isiyo ya kawaida ikinyesha katika kisiwa cha Sumatra.

Kanda za video zinaonyesha mafuriko yakivunja kingo za mito, wakaazi wakiingia kwenye maji hadi kifuani, na magari na nyumba zikikaribia kuzama kabisa katika mitaa iliyofurika - huku sehemu za paa zao zikiwa zimesalia tu kuonekana.

Waokoaji wanakimbia kuwaleta watu zaidi kwenye maeneo salama, lakini kukatika kwa umeme na maporomoko ya matope kumetatiza juhudi zao za kutafuta.

Wakati huo huo, Sri Lanka pia inakabiliwa na maafa mabaya zaidi ya hali ya hewa katika miaka ya hivi karibuni, na takriban watu 56 wamekufa na 21 hawajulikani walipo baada ya mafuriko na maporomoko ya ardhi katika maeneo kadhaa ya nchi.

Watu 21 waliuawa katika wilaya ya kati inayolima chai ya Badulla wakati maporomoko ya ardhi yalipoanguka kwenye nyumba zao usiku kucha, Kituo cha Kudhibiti Maafa (DMC) kilisema katika taarifa.

Video zinazoonekana kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha nyumba zikisombwa na maji huku mafuriko yakipita mijini na huduma nyingi za treni zikifutwa kote nchini.

Sri Lanka sasa inajizatiti kukabili hali mbaya ya hewa siku ya Ijumaa huku Kimbunga Ditwah kikisonga kando ya pwani yake ya mashariki.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code