Ugonjwa wa amoeba (amoebiasis) kwa watoto husababishwa na kimelea kinachoitwa Entamoeba histolytica. Huathiri zaidi utumbo mpana na wakati mwingine ini.
Sababu kuu za maambukizi ya Amiba kwa Watoto
1.Kunywa maji machafu au yasiyochemshwa
2.Kula chakula kisichoandaliwa vizuri(kichafu)
3.Kutokunawa mikono
4. Au kwa ujumla Mazingira yenye usafi duni
Dalili za Amoeba kwa Watoto
1. Dalili za kawaida
-Kuharisha au kujisaidia choo kama makasi
-Maumivu ya tumbo, hasa upande wa chini
-Kupungua kwa hamu ya kula
-Kupata Kichefuchefu na kutapika
-Maumivu ya tumbo yanayokuja na kuondoka (cramps)
2. Dalili Zinazoonyesha maambukizi yamezidi
-Kuharisha damu au kamasi yenye damu
-Kupata Homa
-Kuwa na dalili za Upungufu wa maji (dehydration) kama vile:
- midomo kukauka,
- macho kuingia ndani zaidi,
- mtoto kuwa mlegevu
- au Mwili kukosa nguvu n.k.
-Kupungua uzito endapo ugonjwa umedumu
3. Dalili adimu lakini hatari
Amoeba ikivamia ini dalili hizi huweza kujitokeza:
-Kupata Maumivu upande wa juu kulia tumboni
-Kupata Homa za mara kwa mara
-Mwili kukosa nguvu kabsa
Matibabu (Muhimu Sana)
Kwa watoto wenye shida hii, matibabu lazima yatolewe na mtaalam wa afya.
Au kwa Ushauri Zaidi au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.









image quote pre code