Waliokufa kwa kimbunga nchini Ufilipino wafikia 140

Waliokufa kwa kimbunga nchini Ufilipino wafikia 140

#1

Watu wasiopungua 140 wamefariki dunia baada ya mafuriko makubwa yaliyotokana na kimbunga Kalmaegi nchini Ufilipino. Mamlaka nchini humo zimesema watu wengine 127 hawajulikani walipo.



Maji yaliyofurika yaliyoelezewa kuwa yasiyo ya kawaida, yalitiririka kwa kasi katika miji kadhaa ya mkoa wa Cebu na kuyasomba magari, nyumba na makontena makubwa ya mizigo. 

Kimbunga Kalmaegi chaelekea Vietnam

Taarifa zaidi zinasema kasi ya upepo ulioambatana na kimbunga hicho imeongezeka Alhamisi kuelekea Vietnam kunakohofiwa kutokea uharibifu zaidi baada ya mafuriko ya wiki nzima ambayo yameshasababisha vifo vya watu 47.

Kimbunga hicho kinatajwa kuwa ndicho kibaya zaidi kwa mwaka 2025 kwa mujibu wa kanzidata ya majanga inayofahamika kama EM-DAT.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code