Maporomoko hayo ya matope yamechangiwa na kuendelea kunyesha kwa mvua kubwa
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kipchumba Murkomen, ametoa wito kwa wakaazi katika eneo hilo kuwa waangalifu hasa wale wanaoishi sehemu za milima na kuwagiza mamlaka katika eneo hilo kuwahamisha watu walio hatarini hadi maeneo ya juu.
Kwa sasa polisi na shirika la msalaba mwekundu wanapiga doria katika eneo hilo kwa kutumia ndege aina ya helikopta ili kuweza kuwatambua waathiriwa waliohai walipo.
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amesema kwamba vikosi vya kitengo maalum cha uokoaji kutoka jeshi la Kenya KDF linashirikiana na polisi , wahudumu wengine wa dharura kusaidia kuwatafuta waliopotea na pia kutafuta ikiw akuna miiili iliyozikwa ardhini na tope.
Mvua kubwa inaripotiwa kunyesha usiku wa kuamkia Jumamosi Novemba 1 na kusababisha maji kujaa katika maeno yaliyo chini yam ilima katika bondo hilo la Kerio.
Usafiri katika eneo la tukio umesimamishwa kwa muda kwa sababu ya maji yaliyojaa kote na mapormoko ya ardhi. Wakazi wameombwa kutopanga safari ambazo zio za dharura kwa sasa hadi hali iwe nzuri. Maji wa mafuriko na maporomoko ya usiku wa kuamkia Jumamosi hii yalisomba baadhi ya nyumba katika eneo hilo.
Familia zilizoathirika zinapokea misaada ya mahali pa kulala, maji safi, dawa na chakula.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Kenya imesema kwamba maporomoko ya ardhi huenda yakatokea katika kaunti angalau 30 ambazo zinashuhudiwa viwango vya juu vya mvuwa.
Ajali hii inatokea siku chache tu baada ya ajali inyine kutokea nchini Uganda ambapo watu tisa walifariki, wakiwemo Watoto waliokutwa na mauti walipozikwa na mapormoko ya ardhi yaliyotokea katika maeneo mawili yaliyipo mashariki mwa Uganda.
Mapormoko hayo yalitokea katika miji ya milimani ya Bukwo na Kween usiku wa Jumatano October 29 kutokana na mvua kubwa iliyonyesha magharibi mwa Kenya na Mashariki mwa Uganda










image quote pre code