Watu takriban 94 wamefariki dunia huku waokoaji wakiendelea kutafuta wengine angalau 300 ambao bado hawajulikani waliko, mamlaka ya Hong Kong imesema.
Mamlaka zinasema wavu na karatasi za plastiki kwenye madirisha ya majengo huenda zilisababisha moto kuenea haraka zaidi.
Uchunguzi juu ya ufisadi umeanzishwa kufuatia kukamatwa kwa watu watatu wanaosimamia kazi za ukarabati katika jengo hilo.
Wakaazi kadhaa wamefichua katika mahojiano kuwa kengele ya kutoa tahadhari ya moto haikulia moto huo ulipozuka.
Idara ya zima moto ilisema wazima moto walikabiliwa na changamoto kubwa kujaribu kuwaokoa wakaazi, pamoja na joto la juu na kuanguka zaidi kwa ghorofa.
Mamia wamehamishwa hadi kwenye makazi ya muda huku wengine wakipelekwa kwenye nyumba za dharura.
Moto huo umekuwa mbaya zaidi Hong Kong katika takriban miaka 80 - ikipita idadi ya walioathirika na moto huo mnamo mwezi Agosti 1962 katika wilaya ya Sham Shui Po ambayo iliua watu 44.









image quote pre code