WHO yazindua mwongozo wa usimamizi wa ugonjwa wa kisukari kwa wajawazito

WHO yazindua mwongozo wa usimamizi wa ugonjwa wa kisukari kwa wajawazito

#1

Mtaalamu wa afya akikagua kiwango cha sukari katika damu ya mwanamke mjamzito na mwenye ugonjwa wa kisukari katika Kituo cha Usaidizi wa Kisukari na Endocrinology huko Bahia, Brazili.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO leo limezindua mwongozo wake wa kwanza wa kimataifa kuhusu usimamizi wa ugonjwa wa kisukari kwa wajauzito, ugonjwa unaoathiri takribani mwana mke mmoja mwenye mimba moja kati ya wanawake sita—sawa na wanawake milioni 21 kila mwaka.

Uzinduzi wa mwongozo huo umefanyika hii leo ikiwa dunia inaadhimisha Siku ya Kisukari Duniani, tarehe 14 Novemba 2025 chini ya kauli mbiu isemayo, “Kisukari katika hatua zote za maisha,” inasisitiza haja ya huduma jumuishi na mazingira yanayowawezesha watu wote wanaoishi na kisukari kujidhibiti na kuishi kwa heshima.

Kisukari cha mimba kisipodhibitiwa ipasavyo, huongeza hatari ya matatizo makubwa kama shinikizo la juu la mimba (pre-eclampsia), vifo vya watoto tumboni, na majeraha wakati wa kujifungua.

WHO inasema tatizo hilo ni kubwa zaidi katika nchi za kipato cha chini na cha kati ambako huduma maalum hupatikana kwa shida.

“Hii ni mara ya kwanza kwa WHO kutoa kiwango maalum cha huduma kwa usimamizi wa kisukari wakati wa ujauzito,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus. “Mwongozo huu umejengwa katika uhalisia wa maisha ya wanawake na unatoa mbinu madhubuti, zenye ushahidi, za kuhakikisha kila mwanamke anapata huduma bora, popote alipo.”

Mwongozo huo una mapendekezo 27, ikiwemo:

Ushauri wakipekee kwa kila mgonjwa kuhusu lishe, mazoezi na viwango vinavyolengwa vya sukari;

Uchunguzi wa mara kwa mara wa sukari kwa wanawake wote wenye kisukari, kliniki na nyumbani;

Matibabu ya kipekee kwa kila mgonjwa kulingana na aina ya kisukari—aina ya 1, aina ya 2 au kisukari cha mimba;

Huduma ya kitaalamau zaidi ya kitabibu kwa wanawake wenye kisukari kabla ya ujauzito.

WHO inasema mwongozo huu ni hatua muhimu katika kuimarisha afya ya mama na kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, huku ikisisitiza umuhimu wa kuunganisha huduma za kisukari katika huduma za kawaida za wajawazito.

Dunia ina zaidi ya watu milioni 800 wanaoishi na ugonjwa wa kisukari, na ongezeko kubwa likiripotiwa katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code