Zaidi ya watu 900,000 wamehamishwa nchini Ufilipino kabla ya Kimbunga Fung-wong, ambacho kinatarajiwa kutua nchini humo jioni ya leo, Jumapili, Novemba 9, 2025.
Kimbunga hicho kimepandishwa hadhi na kuwa kimbunga kikuu (super typhoon) chenye kasi ya upepo wa wastani wa kilomita 185 kwa saa na vipindi vya upepo mkali vinavyofikia hadi kilomita 230 kwa saa, kwa mujibu wa Idara ya Hali ya Hewa ya Taifa ya nchi hiyo.
Mkoa wa Mashariki wa Bicol ndiyo ulikuwa wa kwanza kupigwa moja kwa moja na kimbunga hicho Jumapili asubuhi, huku kisiwa cha Luzon — ambacho ndicho kitovu cha makazi ya watu wengi nchini humo — kikitarajiwa kuathiriwa kufikia Jumapili usiku.
Fung-wong, kinachojulikana kitaifa kama Uwan, kimekuja siku chache tu baada ya kimbunga kingine, Kalmaegi, kuleta uharibifu mkubwa na kusababisha vifo vya takribani watu 200.
Shule kadhaa zimefuta masomo ya Jumatatu au kuhamishia masomo hayo mtandaoni, huku takribani safari za ndege 300 zikifutwa.









image quote pre code