Zungu atangazwa Mshindi wa Kura za Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Zungu atangazwa Mshindi wa Kura za Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

#1

Mbunge Mteule wa Jimbo la Ilala, Dar es salaam Mussa Azzan Zungu ameibuka Mshindi wa kinyang’anyiro cha Kiti cha Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambapo anakwenda kuwa Spika wa tisa wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zungu ameibuka Mshindi na kutangazwa hii leo Novemba 11, 2025 kwa kupata kura 378 dhidi ya Wapinzani wake Veronica Charles Tyeah wa Chama cha NFA ambaye hajapata kura, Anitha Alfan wa Chama cha NLD. aliyepata kura moja, Ndoge Said Ndonge wa AFP aliyepata kura moja pamoja na Amin Alfred Yango wa ADC ambaye hajapata kura.

Zungu amekuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 20 hadi sasa ambapo aliingia Bungeni rasmi mwaka 2005 na kushika nyadhifa mbalimbali kama Mwenyekiti wa Bunge 2012-2021, Naibu Spika 2022 mpaka 2025 na amefanya kazi na Maspika wanne wa Bunge hilo.

Spika huyu mpya ana elimu ya Uhandisi wa Ndege na amepata mafunzo hayo Nchini Tanzania pamoja na Nchini Canada ambapo alihitimu mwaka 1982 na amekuwa pamoja na shahada nyingine za maswala ya Diplomasia ambazo alihitimu mwaka 2007 na mwaka 2021.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code