Wabunge wa Chama cha Mapinduzi wamepitisha jina la Mbunge wa Ilala Kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Azzan maarufu ‘Zungu’ kuwania kiti cha Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zungu amechaguliwa na Wabunge hao wa CCM kwa kura 348 ziliopigwa na kumbwaga mpinzani wake Stephen Masele aliyeambulia kura 16 huku kukiwa hakuna kura iliyoharibika.
Zungu ambaye alikuwa Naibu Spika wa Bunge lililopita chini ya Tulia Ackson anatarajiwa kuwa kuwa Spika Bunge la 13 linalotarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumanne ijayo, Novemba 11,2025.
Awali Spika Tulia ambaye alichukua fomu kuomba ridhaa kutoka Chama chake Cha Mapinduzi(CCM), kutetea kiti hiko lakini baadae alitangaza kujitoa katika kinyang’anyiro hiko siku moja kabla ya uchaguzi huo kufanyika.









image quote pre code