Asafiri Peke yake takribani saa 14 ndani ya Ndege ya Emirates
Abiria mmoja wa Emirates amezua gumzo mtandaoni baada ya kusafiri kutoka Brisbane hadi Dubai kwenye ndege yenye safari ya takribani saa 14 huku akijikuta peke yake kwenye daraja la uchumi.
Pamoja na hali hiyo ya kipekee, abiria huyo aliwaomba wahudumu apewe ruhusa ya kwenda daraja la juu, lakini ombi lake halikukubaliwa. Wahudumu walimweleza kuwa kwa kuwa alishakuwa na nafasi kubwa ya kulala na kupumzika, kupanda daraja la juu kusingeleta faida kubwa zaidi.
Hata hivyo, abiria huyo alisema hakujutia maamuzi hayo, akidai alipata usingizi wa kutosha na alifika Dubai akiwa hajachoka sana kutokana na utulivu wa ndege nzima.
Tukio hili limeibua mjadala kuhusu sera za mashirika ya ndege kuruhusu wateja kupanda daraja la juu, hasa wakati viti vya daraja la juu vikiwa wazi. Lakini kwa wasafiri wengi, kupata nafasi tupu kiasi hiki kwenye safari ndefu ni kama kushinda bahati nasibu, ni ndoto ambayo mara chache hutokea kwenye Safari za angani.









image quote pre code