Diwani wa kata ya Mchikichini Nurdin Bilal Juma, maarufu kama Shetta, ametangazwa rasmi kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam leo Desemba 04, 2025, baada ya kupata ushindi katika kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji.
Shetta alipata jumla ya kura 48 za ndiyo kati ya 51 zilizopigwa, huku kura moja ikiharibika, hivyo kumpa ushindi wa kishindo katika nafasi hiyo muhimu ya uongozi.
Katika uchaguzi huo huo, John Mrema alichaguliwa kuwa Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kupata asilimia 96 ya kura, sawa na kura 49 kati ya 51, huku kura moja ikiharibika.
Kikao hicho kimeashiria rasmi kuanza kwa majukumu ya viongozi hao wapya katika kuongoza na kusimamia maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam.









image quote pre code