Je ni tatizo,Kwenda haja kubwa mara tu baada ya kula chakula?

Je ni tatizo,Kwenda haja kubwa mara tu baada ya kula chakula?

#1

Hitaji la kwenda chooni dakika chache tu baada ya kula ni tatizo ambalo watu wengi hukabiliana nalo kila siku.

Hili pia linaibua swali akilini, je, chakula tulichokula kimemeng'enywa ipasavyo?

Kulingana na wataalamu wa matibabu, moja ya sababu za haya ni kula kiasi kidogo wakati wa kazi na kula vitu vingi unavyopenda wakati wa likizo.

Lakini swali ni, je, ni kawaida kujisaidia haja kubwa mara baada ya kula au ni ishara ya ugonjwa?

Daktari bingwa wa magonjwa ya utumbo, Dkt. Mahadevan, anasema, "hitaji la kwenda chooni mara baada ya kula chakula inaitwa 'gastrocolic reflex'. Lakini watu wengi wana dhana potofu kwamba chakula kinacholiwa mara moja huwa kinyesi? Ilhali sivyo."

Je, chakula tunachokula hubadilika kuwa kinyesi kwa haraka?

Kuna matatizo kadhaa ambayo yanaweza kuhusishwa na ugonjwa wa utumbo

Kulingana na utafiti, kwa kawaida huchukua saa 10 hadi 73 kwa chakula kutoka mwilini kama kinyesi. Hii inaitwa 'muda wa kusafirisha chakula'.

Hata hivyo, wakati huu unategemea mambo mengi, kama vile umri wa mtu, jinsia, uzito na lishe.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code