Mapumziko ya Siku Mbili kwa Sababu ya Hedhi

Mapumziko ya Siku Mbili kwa Sababu ya Hedhi

#1

Serikali ya Kaunti ya Nairobi nchini Kenya imeidhinisha rasmi utaratibu wa kutoa siku mbili kila mwezi za kupumzika kwa sababu ya hedhi kwa wanawake wafanyakazi, kama sehemu ya mfumo wa rasilimali watu wa kaunti hiyo.

Uamuzi huu umefikiwa baada ya kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Gavana wa jimbo hilo Johnson Sakaja,

kilichopendekeza kuingiza usaidizi wa afya ya hedhi katika sera za rasilimali watu, kwa lengo la kuboresha ustawi wa wafanyakazi na kuongeza utendakazi wawanawake kazini.

Taarifa ya kaunti inabainisha kuwa changamoto za afya ya hedhi, hususan dysmenorrhea (maumivu makali ya hedhi), huathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa wanawake na utendaji wao kazini.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code