Mchezaji nyota Neymar anatarajiwa kumuona 'daktari wa miujiza' ili kutibu jeraha la goti

Mchezaji nyota Neymar anatarajiwa kumuona 'daktari wa miujiza' ili kutibu jeraha la goti

#1

Mchezaji nyota Neymar anatarajiwa kumuona 'daktari wa miujiza' ili kutibu jeraha la goti

Ripoti zinasema;Nyota wa Brazil, Neymar anatarajiwa kumuona 'daktari wa miujiza(miracle doctor),Mtaalam wa Viungo kwa lengo la kutibu majeraha yake na kufufua matumaini yake ya kushiriki Kombe la Dunia.

Winga huyo wa zamani wa Barcelona na PSG amekosa jumla ya michezo 89 tangu ahamie Al Hilal mwaka 2023 na kisha klabu yake ya utotoni Santos mapema mwaka huu.

Vipindi virefu vimemzuia kuisaidia timu ya Serie A ya Brazil, licha ya kufunga mara 11 na kutoa pasi nne za mabao msimu uliopita huku Santos ikiepuka kushuka daraja.

Katika juhudi kubwa za kuongeza nafasi zake za kushiriki katika kile kinachoweza kuwa Kombe lake la mwisho la Dunia, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 anasemekana kutafuta msaada wa mtaalamu wa viungo wa Brazil Eduardo Santos.

Changia Mada hapa(Reply)

image quote pre code