Sababu za Mtoto kutokaza shingo,Shingo kulegea hizi hapa

Sababu za Mtoto kutokaza shingo,Shingo kulegea hizi hapa

#1

Sababu za Mtoto kutokaza shingo,Shingo kulegea hizi hapa

Hapa chini nimekuletea sababu kuu zinazoweza kumfanya mtoto asikaze shingo (neck control kuchelewa). Nitakupa pia dalili za tahadhari na muda ambao kawaida shingo inapaswa kukaza.

Kawaida Mtoto Anakaza Shingo Lini?

Miezi 2–3: Anapaswa kuanza kuinua kichwa kidogo akiwa tumbo.

Miezi 4: Aweze kushika kichwa bila kuanguka.

Baada ya miezi 5: Asiwe bado analegea kabisa.

Sababu za Mtoto Kutokukaza Shingo

1. Udhaifu wa misuli (Muscle weakness)

Hii ndiyo sababu ya kawaida. Misuli ya shingo inakuwa haijaimarika vizuri.

2. Kukaa muda mwingi mgongoni

Mtoto akikaa muda mwingi mgongoni bila kufanyishwa tummy time(kuwekwa eneo la tumboni),kupakatwa na kupata Support ya mikono, anaweza kuchelewa kuimarisha misuli ya shingo.

3. Kuzaliwa kabla ya wakati (prematurity)

Watoto njiti mara nyingi huchelewa milestones kama kukaza shingo.

4. Kuwa na matatizo yanayosababisha udhaifu wa misuli (Hypotonia)

Hii husababisha mwili kuwa “legelege”. Inaweza kusababishwa na:

  • matatizo ya mishipa ya fahamu (neurological issues),
  • genetic syndromes,
  • matatizo ya ukuaji wa ubongo.n.k.

5. Ugonjwa uliopata wakati wa kuzaliwa

Mfano: upungufu wa oksijeni wakati wa kuzaliwa (birth asphyxia),au kuugua magonjwa mengine,inaweza kuchelewesha hatua za ukuaji kwa Mtoto 

6. Ugonjwa wa mifupa ya shingo (Torticollis / neck stiffness)

Mtoto anaweza kushindwa kugeuza au kuikaza shingo vizuri.

7. Maambukizi makali au utapiamlo

Severe infections au lishe duni vinaweza kuchelewesha ukuaji wa misuli.

JE,MTOTO WAKO ANA SHIDA HII? KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE +255758286584.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code