WHO,Fedha za dharura zatengwa kwa ajili ya waathirika wa kimbunga Sri Lanka

WHO,Fedha za dharura zatengwa kwa ajili ya waathirika wa kimbunga Sri Lanka

#1

Shirika la Afya Duniani (WHO) leo limetoa dola 175,000 kama mfuko wa dharura kwa ajili ya Colombo, Sri Lanka, kufuatia kimbunga kilichosababisha hali mbaya zinazohatarisha maisha nchini humo. Fedha hizi zitatumika kusaidia huduma muhimu za afya na kuwawezesha wadau kutekeleza shughuli za uokoaji kwa watu waliokumbwa na maafa.

Dkt. Rajesh Pandav, Mwakilishi mteule wa WHO nchini Sri Lanka amesema “Fedha hizi zitatumika kwa ajili ya timu za hatua za haraka ili kusaidia huduma muhimu za afya kwa jamii zilizoathirika, na pia kuimarisha usimamizi wa taarifa za afya na ufuatiliaji, ambavyo ni muhimu kwa kugundua kwa wakati milipuko ya magonjwa na kuwezesha hatua zifaazo.”

Kimbunga Ditwah kilitua nchini Sri Lanka tarehe 28 Novemba na kusababisha mafuriko makubwa, maporomoko ya ardhi, na uharibifu mkubwa wa miundombinu kote nchini. Vifo kadhaa, watu wengi kukosa makazi, na kusitishwa kwa huduma muhimu na shughuli za maisha vimeripotiwa nchi nzima.

Ufadhili wa WHO, sehemu yake ikitoka katika Mfuko wa Dharura wa Afya wa Ukanda wa Asia ya Kusini-Mashariki (SEARHEF), unasaidia gharama za uendeshaji kwa ajili ya kuhamasisha na kupeleka timu za matibabu na afya ya umma za hatua za haraka ambazo zitatoa huduma za majeraha, msaada wa huduma ya kwanza, kuwaelekeza wagonjwa wanaohitaji matibabu hospitalini, na kuhudumia wanawake wajawazito, 

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code