Ratiba ya vikao vya Kitaifa vya Chama,uteuzi wa Wagombea Ubunge CCM Yatolewa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa taarifa kuwa ratiba ya vikao vya Kitaifa vya Chama, vitakavyofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitafanyika August 21, 2025, kikifuatiwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa kitakachofanyika August 23, 2025.
Taarifa iliyotolewa leo August 17,2025 na Katibu wa Itikedi na Uenezi wa CCM Taifa, Amos Makalla imesema Ajenda ya Vikao hivyo itakuwa ni uteuzi wa Wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum na vikao vyote vitafanyika jijini Dodoma".
image quote pre code