Mwigizaji Mkongwe na Maarufu nchini Tanzania aitwae Grace Mapunda amefariki dunia
Mwigizaji Mkongwe na Maarufu nchini Tanzania aitwae Grace Mapunda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Aziz Ahmed ambaye ni Muongozaji wa Tamthilia ambaye alikuwa akifanya naye kazi kwa ukaribu kwa muda mrefu “Ni kweli amefariki usiku wa kuamkia leo Mwananyamala Hospitali, alikuwa anasumbuliwa na nimonia”
“Hajaumwa muda mrefu aliletwa Hospitali juzi kisha jana tukaja kumuona ila usiku wa kuamkia leo ndio hivyo tena, msiba upo nyumbani kwake Sinza Vatcan” —— #MillardAyoUPDATES #RIPGraceMapunda #TutaonanaBaadae
Tasnia ya Uigizaji nchini imepata pigo kubwa baada Muigizaji mashuhuri na mkongwe Tanzania @grace_mapundal kufariki Dunia asubuhi ya kuamkia leo.
Grace atakumbukwa kutokana na uhodari wake katika sanaa ya Uigizaji kwa kuuvaa uhusika katika filamu zake nyingi alizowahi kucheza na katika miaka ya hivi karibuni alipata kuigiza kama "Tessa" kwenye tamthilia ya 'Huba'
GRACE MAPUNDA NI NANI?
Grace Mapunda (maarufu kama Mama Kawele) ni mwigizaji wa filamu za Tanzania (Swahiliwood), anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuigiza filamu za hisia na hii ni kutokana na kuwa makini katika kuwakilisha uhusika halisi japo anaonekana kuzipatia filamu za aina hiyo.[1]
Grace Mapunda amebarikiwa kuwa na watoto wawili (Happiness pamoja na Ritha) ambao baba yao alifariki siku za nyuma. Happiness huiigiza na kuimba, aliwahi kuigiza na mama yake katika filamu ya Fake Smile. Ritha naye ni mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya.[2]
Filamu alizoigiza ni pamoja na House of death, hard price, nilindiwe, Kichupa, Majuto, Mwaka wa Hasara, chloroquine love, Chungu ya Nafsi, poor Minds, Jibu la ndoto, Back to life na zingine nyingi[3]
Via;Wikipedia; https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Grace_Mapunda#:~:text=Grace%20Mapunda%20(maarufu%20kama%20Mama,kuzipatia%20filamu%20za%20aina%20hiyo.
Pembe amefariki dunia,Msanii wa vichekesho wa kitambo
Mwigizaji na Mchekeshaji Mkongwe Nchini Tanzania, Mzee Yusuph Kaimu maarufu Pembe amefariki dunia jioni ya leo October 20,2024 katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa mtu wake wa karibu, Pembe amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Dar, Francisco Mwinuka almaarufu Pierre, amethibitisha na kueleza kuwa kwa sasa anaelekea Hospitali ya Temeke na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Aliekua Kocha wa Mamelodi afariki Dunia
Aliekua kocha wa Mamelodi Sundowns na mchezaji wa zamani wa Fc Barcelona na timu ya Netherlands Johan Neeskens amefariki dunia siku ya tarehe 6-10-2024.
Johan Neeskens amefariki ghafla mara baada ya kutoka Algeria,Johan Neeskens alikua Algeria akihudumu kama mtoa elimu ya ukocha kwenye program ya KNVB Coach programs,akiwa kwenye shughuli zake za ukocha alianza kujiskia vibaya na kuumwa ghafla.
Madaktari wa dharura walifika haraka sana lakini huduma ya kwanza haikuweza kuokoa maisha ya Johan Neeskens,Johan ameacha mke anefahamika kama Marlis na watoto wake.
Johan Neeskens ameshinda makombe(mataji) 49 akiwa na timu ya taifa ya Netherlands,Johan Neeskens amefariki akiwa na umri wa miaka 73.
Dida shaibu afariki dunia
Mtangazaji Dida Shaibu Afariki Dunia
Mtangazaji maarufu nchini, Khadija Shaibu almaarufu Didah amefariki dunia jioni ya leo, Oktoba 4, 2024.
Taarifa za kifo cha Didah zimethibitishwa na mtangazaji mwenzake ambaye pia ni mtu wake wa karibu, Maulid Kitenge kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Mtangazaji huyo wa Wasafi FM kupitia kipindi cha 'Mashamsham', Khadija Shaibu maarufu kama Dida amefariki Dunia usiku huu wa leo Ijumaa, Oktoba 4, 2024 baada ya kuugua na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na mtangazaji mwenzake, Maulid Baraka Kitenge kupitia mitandao yake ya kijamii.
Kitenge ameandika; “Dida shaibu wa Wasafi FM amefariki dunia."
Didah amefikwa na umauti akiwa na umri wa miaka 42, ambapo kifo chake kimetokea siku kumi na sita (16) toka Wafuasi wake washuhudie ukimya wake katika mitandao ya kijamii ambapo chapisho lake la mwisho mtandaoni lilikuwa Septemba 19, 2024 ambapo aliweka picha yake akiwa kwenye gari ikisindikizwa na wimbo wa Martha Mwaipaja “Amenitengeneza".
Kabla ya kutua Wasafi, Dida alikuwa akifanya kazi ya utangazaji katika kituo cha Times FM kupitia kipindi cha Mirindimo.
Queen Margrethe wa Denmark amelazwa hospitalini baada ya kuanguka
Malkia Margrethe wa Denmark amelazwa hospitalini kufuatia kuanguka katika Jumba la Fredensborg.
Malkia mwenye umri wa miaka 84, yuko katika hali nzuri, lakini atasalia hospitalini kwa ufuatiliaji, taarifa kutoka kwa ikulu ilisema.
Margrethe, binamu wa tatu wa Malkia Elizabeth, aliratibiwa kushiriki katika hafla ndani ya Chuo Kikuu cha Aarhus siku ya Ijumaa lakini sasa amejiondoa.
alionekana mara ya mwisho Jumatatu alipokuwa akihudhuria Tuzo za Rungstedlund 2024 kwenye Jumba la Makumbusho la Karen Blixen.
Margrethe alishangaza taifa kwa tangazo la kutekwa nyara kwake wakati wa kipindi chake cha televisheni cha moja kwa moja cha Mkesha wa Mwaka Mpya.
Siku 14 tu baadaye, Margrethe, aliyetawala kwa miaka 52, alitia saini kiti cha ufalme kwenye mkutano wa Baraza la Serikali, na mwanawe, Frederik, akatawazwa kuwa Mfalme wa Denmark.
Alisema moja ya sababu iliyomfanya kuchagua kujiuzulu ufalme ni kwa sababu ya maswala ya kiafya, na kuongeza kuwa alifanyiwa upasuaji wa mgongo mnamo Februari 2023.
Alisema: 'Ilikwenda vizuri, shukrani kwa wahudumu wa afya wenye ujuzi ambao walinihudumia. Bila shaka, operesheni hiyo pia ilizua kufikiria juu ya siku zijazo - ikiwa wakati ulikuwa umefika wa kuacha jukumu hilo kwa kizazi kijacho.
Source:LIB
Kaka wa Michael Jackson afariki Dunia kwa mstuko wa moyo.
Kaka wa marehemu Michael Jackson, aitwaye Tito Jackson, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70.
Tito pia alikuwa mwanamuziki katika kundi la familia la The Jackson 5, ambalo Michael Jackson alianza kulitumikia tangu akiwa na miaka sita.
Taarifa za kifo chake zimetolewa na Siggy Jackson, ambaye ni mpwa wake kupitia jarida la 'PEOPLE', zikieleza kuwa Tito Jackson amefariki dunia siku ya jana Septemba 15 kwa mstuko wa moyo.
Kupitia kundi la The Jackson 5, Tito alipata umaarufu katika miaka ya 1970 kutokana na nyimbo kama "I Want You Back," "ABC," na "I'll Be Therena."
Hata hivyo, katika kundi hilo alikuwa na uwezo wa kupiga gitaa na kuandika nyimbo ambazo zilisaidia kukuza kundi hilo.
Tito baadaye alijitosa kufanya kazi za peke yake na kufanikiwa kuwa na albamu kama "Tito" (1978) na "I’m a Winner" (1979).
Mbali na kazi za muziki, Tito alikuwa akijihusisha na shughuli za jamii, kama vile kupigania haki za watu na msaada kwa vijana.