Mjamzito kukojoa mara kwa mara
Nini kinasababisha mama mjamzito kukojoa mara kwa mara? fahamu hapa, Zipo sababu kuu mbili.
Katika hatua za kwanza za Ujauzito, mabadiliko ya vichocheo mwilini yaani hormone changes huongeza hali ya mama mjamzito kukojoa mara kwa mara,
Baadaye katika ujauzito, uterasi yako (tumbo la uzazi) linakuwa kubwa ili kumhifadhi mtoto wako anayekua. Kadri mtoto anavyokuwa ndivo huweka shinikizo zaidi kwenye kibofu cha mkojo, Hii inasukuma kibofu cha mkojo au kukigandamiza pamoja na kusababisha eneo au room ya kibofu cha mkojo kupungua, Sababu hii husababisha kibofu kushindwa kukaa na mkojo mwingi au kwa muda mrefu, na hapa ndipo Swala la kukojoa mara kwa mara hutokea.
Kukojoa mara kwa mara kunaweza kuanza ndani ya wiki kadhaa baada ya mimba kutungwa. Ingawa mjamzito anaweza kukojoa mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya homoni, anapaswa kushauriana na daktari wake iwapo atapata maumivu wakati wa kukojoa au dalili nyingine za maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI).
Kukojoa mara kwa mara ni ishara ya kawaida kwa ujauzito. Mjamzito kukojoa mara kwa mara kwa wiki za mwanzoni hutokea kutokana na kuongezeka kwa viwango vya homoni za projesteroni pamoja na human chorionic gonadotropin (hCG).
Ingawa baadhi ya wajawazito wanaweza kupata mabadiliko madogo, wengine wanaweza kuhisi haja ya kwenda kukojoa mchana na usiku.
Frequency pia ya kukojoa mara kwa mara inaweza kuongezeka tena baadaye katika ujauzito wakati mtoto akiendelea kukua na tumbo la uzazi au uterasi kuongezeka ukubwa, ambapo husababisha shinikizo kwenye kibofu cha mkojo.
Mjamzito kukojoa mara kwa mara si kawaida endapo; kunaambatana na dalili zingine zisizozakawaida kama vile homa au kuhisi baridi sana,kuhisi hali ya kuungua au maumivu wakati wa kukojoa, Hapa unapaswa kutafuta matibabu mara moja kwa sababu inaweza kuwa maambukizi ya njia ya mkojo (UTI). Dalili zingine zinaweza kujumuisha maumivu ya mgongo,misuli au viungo vya ujumla n.k.
Ukiona dalili hizi hakikisha unatafuta Msaada mapema au;
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
MJAMZITO KUKOJOA MARA KWA MARA
Wanawake baada ya kupata ujauzito huweza kupatwa na hali ya kukojoa mara kwa mara,
Kukojoa mara kwa mara kwa mwanamke mjamzito wakati mwingine inaweza ikawa ni kawaida kabisa kama hakuna maambukizi kwenye njia ya mkojo yaani UTI,
Kwanza kabisa kitu muhimu cha kufahamu ni kwamba Mfuko wa uzazi (uterus) upo karibu kabisa na mfuko wa mkojo (urinary bladder)
Kwa ukaribu huu wakati mtoto anakuwa kichwa chake au sehemu nyingine ya mwili hutegemea na mlalo wa mtoto huweza kukandamiza kibofu cha mkojo hivyo husababisha mama kuhisi mkojo mara kwa mara.
Kumbuka kuna magonjwa mengine yanaweza kusababisha kukojoa mara kwa mara kama sukari na U.T.I
kwahyo kwa mama mjamzito anayepitia hali hii ni vizuri ukafika katika kituo cha kutolea huduma kwa uchunguzi wa kitaalamu kabisa
KUMBUKA: Kukojoa mara kwa mara asilimia kubwa ni hali ya kawaida kwa mama mjamzito kutokana na sababu hapo juu,
ila sio kila kukojoa mara kwa mara ni kawaida, kufanya vipimo na kujiridhisha ni vizuri zaidi kwako,
#afyaclass #uzazisalama #inawezekana
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.