Madhara Ya Kutofanya Mapenzi Muda Mrefu
Je kuna Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu?
Zipo dhana mbali mbali na sisi pia kama afyaclass,tumepokea maswali mengi sana,Watu wakiuliza kuhusu Yapi ni Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu?
Kuna Nadharia nyingi kwenye Jamii Zetu,wengine wanakuambia usipofanya utakuwa hivi,wengine vile? Je swala hili lipoje? karibu tukufungue macho kitaalam Zaidi.
Katika makala hii tumechambua baadhi ya tips za kukusaidia kujua kuhusu hili la Madhara ya kutokufanya Mapenzi kwa muda Mrefu.
Ukweli ni kwamba hakuna kiwango sahihi cha kufanya Mapenzi kwa mtu, hii huweza kutegemea kati ya mtu na mtu, na kutokufanya Mapenzi kwa muda mrefu hakuwezi kuwa na madhara kwa afya yako,
Soma Zaidi hapa Kujua,...
Nanukuu maneno kutoka kwenye Jarida la afya(medicalnewstoday) Wanasema;
"No one should ever feel obliged to have sex. Avoiding sex will not harm a person’s health, and it may even be healthy".
Hakuna Mtu wakunyooshewa kidole au kuhukumiwa kwa kutokufanya Mapenzi kwa muda mrefu, Kuepuka kufanya Mapenzi hakuwezi kuleta madhara kwa afya ya mtu, na badala yake huweza kuwa afya Zaidi kwake.
Katika Mada hii tunachambua kwa kuangalia Vitu vikuu Viwili;
- Matokeo kwenye Mwili(Physical effects)
- Matokeo kisaikolojia na kwenye Afya ya akili kwa Ujumla(Psycholigical effects&Mental health in general)
Kwa Mujibu wa tafiti za kitaalam,Hata kama mtu hajafanya Mapenzi kwa miezi kadhaa au miaka, hakuna uwezekano wa kugundua athari zozote mbaya za kiafya kwa afya yake au kwenye Mwili wake,
Ingawa utafiti unaonyesha kuwa kufanya Mapenzi mara kwa mara kunaweza pia kuleta faida fulani za kiafya, Faida hizo ni pamoja na:
- Kuboresha Mfumo wa kinga yako ya mwili
- Kupunguza shinikizo la damu
- Kupunguza kiwango cha Stress
- Kupunguza hatari ya kupata magonjwa mbali mbali ikiwemo magonjwa ya moyo n.k
Kwa wanaume, afya ya tezi dume inaweza kuimarika kutokana na kumwaga manii mara kwa mara, Uchunguzi mmoja uliofanywa mwaka 2018 uligundua kwamba; kumwaga mara mbili hadi nne kwa wiki kulihusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume.
Kwa wanawake, Kufanya Mapenzi mara kwa mara -kunaweza kuimarisha misuli ya sakafu ya pelvic inayounga kibofu. Hii inaweza kuboresha utendajikazi wa kibofu cha Mkojo na kupunguza hatari ya kupata tatizo la kushindwa kuzuia Mkojo mwenyewe.
Kwahyo hayo ni Maelezo Mafupi kuhusiana na Matokeo kwenye Mwili wako(Physical Effects.
(2) Matokeo kisaikojolia,au kwenye afya ya Akili(pyscholigical effects)
Utafiti wa mwaka 2020 kutoka kwenye Chanzo kimoja Kinachoaminika ulichunguza tabia za ngono wakati wa kuzuiwa au(lockdown) kwa muda kutokana na COVID-19,
Utafiti huu uliunga mkono madai kwamba kufanya Mapenzi mara kwa mara kulihusishwa na viwango vya chini vya mfadhaiko na wasiwasi(depression,anxiety)n.k.
Hivo kwa Muktadha huu Kufanya Mapenzi mara kwa mara hupunguza tatizo la Wasiwasi,Msongo wa mawazo,pamoja na Mfadhaiko, Ingawa hii ni kweli kwa watu wengine, sivyo ilivyo kwa kila mtu.
Ingawa kutokufanya Mapenzi kwa Muda mrefu ni jambo la hiari, baadhi ya watu wanaweza kuhisi athari mbaya kwenye afya yao ya kiakili;
Kutokufanya Mapenzi kwa muda mrefu kwa baadhi ya Watu kunaweza kuwafanya wahisi kutojiamini au kuwa na wasiwasi,
Lakini Pia Kwa wengine, kujiepusha na kufanya Mapenzi ni muhimu kwa afya nzuri ya akili. Watu wanaweza kujiepusha na ngono kwa sababu nyingi, kwa mfano, kwa sababu wana hamu ndogo ya kufanya mapenzi au hawana kabsa hamu ya tendo la ndoa, hawana wapenzi au wachumba wakufanya nao tendo,au wanachagua tu kutojihusisha kwa kuona bado sio muda sahihi wa kufanya hivo.
Na moja ya Faida kubwa wanayopata ni kujikinga na Magonjwa ya Zinaa kwa Asilimia 100%.
Hakuna kiwango sahihi cha kufanya Mapenzi, hili hutofautiana kati ya mtu na mtu, Na Kutofanya Mapenzi kwa muda mrefu hakutakiwi kuwe na madhara ya kiafya kwako.
Hakuna mtu anayepaswa kujisikia vibaya kwa kutokufanya Mapenzi. Kuepuka kufanya Mapenzi hakutadhuru afya ya mtu, na kunaweza hata kuwa na faida zaidi kiafya.
ANGALIZO; Hapa hatuhalalishi kwamba kukosa hamu ya Tendo la ndoa ni kawaida, hapana! Kama unakosa hamu ya Tendo hakikisha unaongea na wataalam wa afya kwanza huenda una tatizo la kiafya. Na kwa Ushauri Zaidi au Tiba tunaweza kuwasiliana hapa hapa kwa namba +255758286584.
Ingawa hakuna Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu, lakini kutokuwa na hisia za Mapenzi kabsa huweza kuwa tatizo la kiafya ambalo huhitaji Matibabu,
Hivo kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa, huweza kutokana na Sababu mbali mbali ambazo zingine ni lazima upate matibabu ya kitaalam.
Mfano ni matatizo kama Vile; Tatizo la hormone imbalance n.k.
Hitimisho:
Nanukuu maneno kutoka kwenye jarida ya afya(Healthline)kuhusu Mada hii ya Madhara ya kutokufanya mapenzi muda mrefu
Jarida hili linasema"Despite what you may see on TV, there’s nothing wrong with you if you are not having sex all the time. There is also nothing wrong with you if you never have sex".
Licha ya kile unachoweza kuona kwenye TV au vyanzo vingine vya Taarifa, hakuna ubaya kwako ikiwa hufanyi tendo la ndoa kila wakati. Pia hakuna kitu kibaya kwako ikiwa hujawahi kufanya mapenzi kabsa,
Hakuna Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu, na badala yake huweza kuwa faida kwako,
kwani huweza kukupunguzia hatari ya Kupata magonjwa mbali mbali ya Zinaa(Sexual transmitted diseases-STDs)
Ni matumaini yangu kwamba tumejibu vizuri swali hili la;
" Je, Kuna Madhara ya kutokufanya Mapenzi muda Mrefu?".