Kucha kutumika kutambua baadhi ya Magonjwa
Je, unajua kucha zako zinaweza kutumika kutambua dalili za magonjwa mbali mbali? mfano; Ikiwa kucha nyingi ni nyeupe na zina rims nyeusi, hii inaweza kuonyesha matatizo ya ini, kama vile hepatitis n.k Soma zaidi hapa...!!
1.Ikiwa kucha zako zina mstari mmoja ambao umechimba kidogo na upo mlalo(horizontal) huweza kuashiria;
• Tatizo la utapiamlo
• Shida ya measles(surua)
• Kisukari ambacho hakijadhibitiwa(uncontrolled diabetes)
• Shida ya Pneumonia
• Upungufu wa Madini ya Zinc.
2. Kucha kuwa nene na kutuna, kuwa na kitu kama mgongo,huweza kuashiria;
• magonjwa ya moyo(cardiovascular disease)
• magonjwa ya Ini(Liver diseases)
• Shida kwenye mapafu
• Shida ya upungufu wa kinga mwilini(AIDS)
3. Kucha kuingia ndani na kupinda kama Kijiko,huweza kuashiria;
• Upungufu wa damu unaotokana na upungufu wa madini chuma(Iron-deficiency anemia)
• Magonjwa ya Moyo
• shida ya hypothyroidism n.k
4. Kucha kuwa na mistari miwili mlalo, hii huweza kuwa shida ya sumu au Arsenic poisoning
5. Kucha kuwa za njano(yellow nail syndrome), hii huweza kuashiria;
• Shida ya rheumatoid arthritis
• Chronic bronchitis
• Shida ya Pleural effusions n.k