Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa bawasiri na tiba yake,Madhara na Dalili zake



Ugonjwa wa bawasiri na tiba yake,Madhara na Dalili zake

Ugonjwa wa Bawasiri kwa kitaalam Hemorrhoids ni ugonjwa unaohusisha kuvimba na kutuna kwa mishipa kwenye mfereji wa Njia ya haja kubwa, ambapo Mishipa hii husaidia wakati wa utoaji wa kinyesi.

Kwa Lugha nyingine, Bawasiri huhusisha kuvimba kwa mishipa inayojulikana kama Veins kwenye eneo la haja kubwa yaani anus, pamoja na Sehemu ya ndani ya rectum yaani Lower rectum.

Tumezungumzia kuhusu kutanuka na kuvimba kwa mishipa ya Veins, na tumezungumzia habari ya Rectum.

Veins ni nini?

Veins ni mishipa ya damu iliyo katika mwili wako wote ikiwemo eneo hili la Haja kubwa ambayo hukusanya damu isiyo na oksijeni na kuirudisha kwenye moyo.

Je, Rectum ni nini?

Rectum ni sehemu ya chini ya Utumbo mpana au Utumbo mkubwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Colon au Large intenstine, Sehemu hii ina Karibu Cm15 Sawa na Ichi 6 kwa Urefu. Hapa ndipo Uchafu hupokelewa kutoka kwenye Utumbo mpana kisha kuhifadhiwa mpaka hapo ambapo utatolewa nje ya mwili wako kupitia Sehemu ya haja kubwa au Anus.

AINA ZA BAWASIRI(HEMORRHOIDS)

Kulingana na asili ya Bawasiri au hemorrhoids tunaweza kupata aina kuu Mbili za bawasiri
  1. Bawasiri ya ndani
  2. Na Bawasiri ya nje
Bawasiri au Hemorrhoids ikitokea ndani ya rectum hujulikana kama bawasiri ya ndani au kwa kitaalam Internal hemorrhoids

Lakini endapo bawasiri imetokea chini ya ngozi inayozunguka eneo la haja kubwa au Anus hujulikana kama bawasiri ya Nje au kwa kitaalam external hemorrhoids.

Hivo basi, Tunaweza kujua aina za bawasiri uliyonayo kulingana na eneo ilipotokea pamoja na Dalili ulizonazo kwa wakati husika.

DALILI ZA BAWASIRI YA NDANI NA BAWASIRI YA NJE

Watu wengi hawajui kwamba bawasiri zipo za aina kuu mbili,kuna bawasiri ya ndani na kuna bawasiri ya nje.

Na dalili pia za bawasiri hutegemea ni bawasiri ya Nje au ya ndani.

Tuanze na dalili za bawasiri ya nje

1.DALILI ZA BAWASIRI YA NJE(External hemorrhoids)

Aina hii ya bawasiri huhusisha eneo la kuzunguka sehemu ya haja kubwa au Anus. Na dalili zake ni pamoja na;

- Kutokea kwa kinyama au uvimbe eneo la haja kubwa ambacho huonekana kabsa kwa nje,

kinyama hiki unaweza kukishika kabsa na kujua sehemu ya haja kubwa ina kitu

- Mtu kuhisi hali ya miwasho kwenye eneo la haja kubwa

- Mtu kupata maumivu hasa wakati wa kujisaidia haja kubwa

- Mtu kuhisi hali ya kutekenywa au kukereka eneo la haja kubwa

- Kuanza kuvuja damu(Bleeding) au kujisaidia kinyesi kilichochanganyika na damu n.k

Baada ya kuangalia dalili za bawasiri ya Nje, twende moja kwa moja kutazama Dalili za bawasiri ya Ndani kama aina nyingine ya bawasiri

2.DALILI ZA BAWASIRI YA NDANI(Internal hemorrhoids)

Aina hii ya bawasiri hutokea kwenye eneo la ndani la Rectum,

- Na kwa kawaida huwezi kuona au kufeel chochote kwa nje

- Na ni mara chache huweza kuleta kero au usumbufu wowote kwa nje

- Lakini mtu huanza kuhisi hali ya mkazo usio wa kawaida(straining) au Irritation wakati kinyesi kikipita anapojisaidia, na hii ndyo huweza kusababisha;

• Kujisaidia kinyesi chenye damu au kuvuja damu wakati wa kujisaidia pasipo kupata maumivu ya aina yoyote,

• Unaweza kushangaa kuna vidamu damu ambavyo ni Bright red blood kwenye toilet tissue au ndani ya kinyesi

Je,unasumbuliwa na aina yoyote ya bawasiri kati ya hizi?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Hakikisha Unaongea na Wataalam wa Afya

Ikiwa unatokwa na damu wakati wa kwenda haja kubwa au una bawasiri ambazo haziishi baada ya wiki, licha ya kuzingatia kanuni za utunzaji wake ukiwa nyumbani, zungumza na mtoa huduma wako wa afya.

Sio kila kutokwa na damu kwenye njia ya haja kubwa ni kwa sababu ya bawasiri, haswa ikiwa una mabadiliko katika tabia ya kinyesi chako au ikiwa kinyesi chako kinabadilika rangi au hali yake ya kawaida ya kutoka kila siku. 

Kutokwa na damu kwenye eneo la Haja kubwa kunaweza kutokea kwa sababu ya magonjwa mengine, Ikiwemo saratani ya utumbo mpana na saratani ya Sehemu ya haja kubwa.

Tafuta huduma ya dharura ikiwa unatokwa na damu nyingi kwenye eneo la haja kubwa, au una dalili zingine kama vile; maumivu makali ya kichwa,kichwa kuwa kizito, maumivu makali ya tumbo,kupata hali ya kizunguzungu au kuzirai.n.k

SABABU ZA UGONJWA WA BAWASIRI

Mishipa ya Veins inayozunguka njia ya haja kubwa hutanuka kutokana na shinikizo inayopata na inaweza kujitokeza au kuvimba.  Bawasiri au Hemorrhoids inaweza kuendelea kutokana na kuongezeka kwa shinikizo kwenye eneo la rectum kwa sababu mbali mbali Zikiwemo:

  • Hali ya mkazo wakati wa kujisaidia ambayo hutokana na Sababu mbali mbali ikiwemo ya kujisaidia choo kigumu sana.
  • Kukaa kwa muda mrefu hasa wakati wa kujisaidia
  • Kuwa na tatizo la kuharisha kwa muda mrefu yaani chronic diarrhea 
  • Kujisaidia choo kigumu sana au kupata tatizo la constipation.
  • Kuwa na Uzito kupita kiasi au Unene(overweight and Obesity)
  • Kuwa Mjamzito, Wajawazito wengi pia hupata shida hii ya bawasiri hasa kutokana na kuongezeka kwa mgandamizo au shinikizo kwenye eneo hili
  • Kufanya Mapenzi kinyume na maumbile(anal sexual intercourse)
  • Kula vyakula vyenye kiwango kidogo cha nyuzinyuzi yaani low-fiber diet.
  • Kunyanyua Vitu vizito mara kwa mara n.k

Wakati mwingine hakuna Sababu ya moja kwa moja ambayo hujulikana kama chanzo cha bawasiri, lakini mara nyingi Wataalam wa afya huzungumzia sababu kuu kadhaa. Sababu hizi ni pamoja na;

 1. Kupata choo kwa shida au Kupata Choo Kigumu

2. Tatizo la kuharisha kwa muda mrefu, 

3. Kukaa kwa muda mrefu hasa wakati wa kujisaidia

4. Bawasiri au Hemorrhoids pia inaweza kuonekana kwa sababu ya michezo ambayo watu hucheza mfano; kunyanyua Vyuma au vitu vizito,

Wakati kitu kizito kinapoinuliwa, shinikizo la ziada linatumika kwenye eneo hilo hivo kuweza kuchangia tatizo hili.

5. Wanawake wako katika hatari ya kuwa na bawasiri wakati wa ujauzito.

Hii pia hutokea kwa sababu ya kuongezeka kwa shinikizo la kutoka kwa mtoto.  Bawasiri ina uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa sababu tishu zinakuwa dhaifu.

Watu ambao wapo kwenye hatari ya kupata Ugonjwa wa bawasiri

- kuwa kwenye Familia yenye Tatizo hili(Genetics)

Unaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata bawasiri ikiwa wanafamilia wengine, kama wazazi wako, walikuwa nayo.

- Wazee

Wazee wanaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata bawasiri kwa sababu tishu katika eneo la Haja kubwa huwa dhaifu kadri unavyozeeka.

- Wajawazito

Mimba huongeza hatari ya kupata bawasiri kwa njia kadhaa.  Uzito wa Mtoto aliye tumboni huweka shinikizo la ziada kwenye puru yako.  Pia una uwezekano mkubwa wa kupata bawasiri kwa Sababu ya kupata tatizo la Kujisaidia Choo Kigumu.

- Wanaokaa kwa Muda mrefu

Mtindo wa maisha wa kukaa tu, au kazi ambayo lazima ukae kwa muda mrefu, pia huongeza hatari ya kupata bawasiri.  Usipozunguka sana au kufanya mazoezi ya mwili,damu inaweza kujikusanya kwenye eneo lako la Haja kubwa na kuweka shinikizo kwenye mishipa ya damu hapo, Hali hii huongeza hatari ya wewe kupata bawasiri.

Madhara ya Ugonjwa wa bawasiri

Bawasiri inaweza kuleta wasiwasi na maumivu, lakini mara nyingi haisababishi matatizo makubwa.  Mara chache, watu walio na Bawasiri hupata madhara haya:

Upungufu wa damu; Unaweza kupoteza damu nyingi ikiwa una bawasiri ambayo hudumu kwa muda mrefu na inayosababisha kutoka kwa damu nyingi. Hali hii huweza kusababisha upungufu wa damu mwilini

Kuganda kwa damu; Hali ya kuganda kwa damu(Blood clots) huweza kutokea hasa kwa mtu mwenye bawasiri ya nje.

 • Maambukizi; Baadhi ya bawasiri kama bawasiri ya nje huweza kusababisha vidonda ambavyo huwa rahisi kuambukizwa.

Tatizo la Skin tags(kitambaa cha tishu zinazoning'inia kwenye ngozi); Tone la damu kwenye bawasiri yenye mvilio linapoyeyuka, linaweza kuacha sehemu ya ngozi, na eneo hili linaweza kuwasha.

 • Bawasiri zilizofungwa(Strangulated hemorrhoids);

Misuli inaweza kuzuia mtiririko wa damu hadi kwenye bawasiri iliyozidi,prolapsed hemorrhoid. Hii inaweza kusababisha maumivu makali na inahitaji upasuaji.

🔺UTAMBUZI WA UGONJWA WA BAWASIRI

 Bawasiri au Hemorrhoids hugunduliwa na daktari au wataalam wa afya,

Daktari wako atakuuliza kuhusu historia ya Ugonjwa wako, matibabu na dalili ulizo nazo.

Vipimo mbali mbali vitafanyika ikiwemo; kufanya

  • Physical examination; Ambapo daktari huweza kukuangalia eneo la Haja kubwa pamoja na rectum, ili kuona kama kuna uvimbe wowote, au tatizo lingine lolote.
  • Kipimo cha Digital rectal exams;

Hapa Daktari wako atavaa gloves, atapaka mafuta, na kuingiza kidole kwenye puru yako ili kuangalia sauti ya misuli na kuhisi hali yoyote ya uvimbe, au matatizo mengine.

 Uchunguzi wa kuona sehemu na Njia ya haja kubwa kwa undani lazima ufanyike.  katika kufanya uchunguzi wa rectal ambao utasaidia kugundua bawasiri ya ndani, uvimbe, polyps, au jipu,

Uchunguzi huu wa kuona kawaida huhitaji kifaa maalum, kinachoitwa Anoscopy kuingizwa kwenye eneo la haja kubwa.  Utaratibu huu hauna maumivu isipokuwa ugonjwa mwingine umewasilishwa.

 ðŸ”´ MATIBABU YA UGONJWA WA BAWASIRI

 Matibabu ya bawasiri au hemorrhoids yanaweza kufanyika kuanzia nyumbani au hospitalini.  Kawaida, chaguo bora ni kuzuia kuipata.  Moja ya vitu Muhimu ni pamoja na kuongeza unywaji wa Maji mengi na ulaji wa vyakula au matunda yenye asili ya nyuzi nyuzi. 

👉 Hii inamaanisha kula matunda zaidi, mboga mboga, na nafaka nzima.  Watu wengi hawapati Fiber au nyuzi za kutosha katika lishe yao.  Katika hali kama hiyo, virutubisho vya nyuzi, kama vile psyllium au methylcellulose, vinaweza kuwa na faida.

👉 Pia ni muhimu kuongeza unywaji wa maji ya kutosha na kudumisha unyevu.  Inashauriwa kunywa glasi sita hadi nane za maji kwa siku ili kusaidia katika hali hii.

👉 Njia nyingine ya kupunguza hali hii;

  • Loweka eneo lako la haja kubwa katika maji ya Moto ya kawaida ambayo hayatakuunguza kwa dakika 10 hadi 15 mara mbili au tatu kwa siku.  Hii huweza kukusaidia pia.

Matibabu ya Bawasiri

Mbali na vitu vya kula,kufanya na kuzingatia ukiwa nyumbani,Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kama Tiba kwa Mgonjwa wa bawasiri ikiwemo;

  • Matumizi ya dawa mbali mbali za Kupaka(Cream), Na za kuweka Sehemu ya Haja kubwa(suppository)
  • Kutumia dawa za kutuliza maumivu
  • Pamoja na Huduma ya Upasuaji

Jinsi ya Kuzuia Bawasiri(Prevention)

Njia bora ya kuzuia bawasiri ni kuhakikisha kinyesi chako kinakuwa laini ili kipite kwa urahisi.  Ili kuzuia hemorrhoids na kupunguza dalili za hemorrhoids, fuata vidokezo hivi:

 ✓ Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi.

 Kula matunda zaidi kama papai,parachichi,embe,n.k. Pia kula mboga mboga na nafaka nzima.  Kufanya hivyo kunapunguza kinyesi kuwa kigumu na kuongeza wingi wake.  Hii itakusaidia kuepuka matatizo ambayo yanaweza kusababisha hemorrhoids.  Ongeza nyuzinyuzi kwenye mlo wako polepole ili kuepuka matatizo na gesi.

 ✓ Kunywa maji mengi. 

 Kunywa glasi 6 hadi 8 za maji na vinywaji vingine kila siku ili kusaidia kuweka kinyesi kuwa laini.  Kuepuka pombe pia kunaweza kusaidia.

 ✓ Fikiria virutubisho vya nyuzinyuzi.

  Watu wengi hawapati nyuzinyuzi za kutosha katika mlo wao.  Uchunguzi umeonyesha kuwa virutubisho vya nyuzi, kama vile psyllium au methylcellulose (Citrucel), vinaweza kupunguza dalili na hali ya kutokwa na damu kutokana na bawasiri.

 Ikiwa unatumia virutubisho vya nyuzinyuzi, hakikisha unakunywa angalau glasi nane za maji au vinywaji vingine kila siku.  Vinginevyo, virutubisho vinaweza kusababisha kuvimbiwa au kuifanya hali hii kuwa mbaya zaidi.

 ✓ Usijikaze sana wakati wa Kujisaidia. 

 Kujikaza sana na kushikilia pumzi yako wakati wa kujaribu kupitisha kinyesi husababisha shinikizo kubwa kwenye mishipa ya puru ya chini. Hii huweza kuongeza hatari ya wewe kupata bawasiri

 ✓ Fanya MaZoezi ya Mwili.

 Endelea kufanya kazi na mazoezi ili kusaidia kuzuia tatizo la kupata choo kigumu au constipation na kupunguza shinikizo kwenye mishipa.  Mazoezi pia yanaweza kukusaidia kupunguza uzito kupita kiasi ambapo hali hii inaweza kusababisha bawasiri au kuifanya kuwa mbaya zaidi.

Pamoja na Mazoezi unayofanya,epuka kunyanyua vitu vizito sana,na fanya mazoezi kwa kiasi.

✓ Epuka kukaa kwa muda mrefu.  

Kukaa kwa muda mrefu, haswa kwenye choo, kunaweza kuongeza shinikizo kwenye mishipa kwenye njia ya haja kubwa, hali hii inaweza kusababisha bawasiri au kuifanya kuwa mbaya zaidi.

Hitimisho

Ugonjwa wa Bawasiri kwa kitaalam Hemorrhoids ni ugonjwa unaohusisha kuvimba na kutuna kwa mishipa kwenye mfereji wa Njia ya haja kubwa, ambapo Mishipa hii husaidia wakati wa utoaji wa kinyesi.

Kwa Lugha nyingine, Bawasiri huhusisha kuvimba kwa mishipa inayojulikana kama Veins kwenye eneo la haja kubwa yaani anus, pamoja na Sehemu ya ndani ya rectum yaani Lower rectum.

DALILI ZA KUWEPO KWA UGONJWA WA BAWASIRI KWA UJUMLA

 ➖ Dalili za bawasiri ni pamoja na hali ya kuwashwa, kutokwa na damu, uvimbe,hisia ya kuchoma au kuwaka sehemu ya haja kubwa, na kuhisi kama mchanga sehemu ya Haja kubwa.

➖ Wagonjwa pia wanalalamika juu ya usumbufu wa jumla wakiwa wamekaa, kuhisi uwepo kitu ndani ya njia ya haja kubwa.

➖  Bawasiri au  Hemorrhoids inaweza kusababisha kutokwa na damu kwa njia ya haja kubwa

➖ Kupata maumivu sehemu ya haja kubwa

➖ Uwepo wa kitu kama donge la hudhurungi sehemu ya Haja kubwa.Lakini wakati mwingine hemorrhoids za ndani pia zinaweza kuwa chungu sana.  Hii hufanyika kwa sababu hua na kitu kama kitambaa. 

 ➖ Kumbuka maumivu katika eneo karibu na njia ya haja kumbwa yanaweza kuwa ni kwa sababu ya tatizo Lingine, kama michubuko au kuchanika njia ya haja kubwa, tatizo la fistula ya njia ya haja kubwa n.k

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!



Post a Comment

0 Comments